Mwanamke mmoja Kilimanjaro amekamatwa na polisi akidaiwa kumkata mtoto
wake mwenye umri wa miaka nane nyama ya paja na kuichoma mithili ya
mshikaki.
Mwananmke huyo aliyetajwa kwa jina la Dafrosa Massawe anadaiwa kufanya
unyama huo mwishoni mwa wiki na majirani wanasema mama huyo alifanya
hivyo akiwa amelewa.
Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Koka Moita alisema mwanamke huyo
ataendelea kushikiliwa hadi uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika
kabla ya kupelekwa mahakamani.
Akizungumza na Gazeti la MWANANCHI katika hospitali ya Kibosho mtoto
huyo alisema hafahamu kosa alilofanya hadi mama yake ambaye ni
mtengenezaji wa pombe za kienyeji kumfanyia kitendo hicho.
Alisema mama yake alirudi nyumbani usiku na kumkuta amekaa na kumsalimia
kisha akamwomba chakula wakati akijua hakuna na baadae aliingia jikoni
na kuchukua kisu kisha kumkata nyama kwenye paja lake baada ya kumwambia
alishinda na njaa siku nzima.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni