Alhamisi, 11 Septemba 2014
HONGERENI DARASA LA SABA KWA KUHITIMU..
Leo ni siku ya furaha sana kwa vijana wote walio andikishwa shule ya msingi na kuanza darasa la kwanza mwaka 2008,mitihani hiyo iliyoanza tangu jana na kumalizika leo kwenye mida ya saa saba mchana huu wa tarehe 11.09.2014 ,Mitihani iliyo fanyika Tanzania nzima.
Ushahuri kwa wazazi na watoto,shule haijaisha ndio kwanza wanaanza kunawa uso waone vizuri,chonde chonde wasijiingize kwenye vitendo hatarishi na pia wazazi inatakiwa kuwa nao karibu kuliko ilivyo kuwa mwanzo wakiwa shule.
Pia kwa wale wenzangu na mimi wazazi wanao dhani watoto wao wamekuwa na wanaweza anzisha familia zao huo ni unyanyasaji na ni kumuuwa mtoto kimaendeleo hata na wewe mzazi pia,mwache mtoto aendelee na masomo ya sekondari hata kama hana uwezo darasani itamsaidia kuliko uwamuzi mwingine wowote.nawatakia mapumziko mema lasaba wotemlio maliza leo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni