THE EVENT

Jumanne, 9 Desemba 2014

JAMAA MMOJA AFANYA UTAFITI NDANI YA TUMBO LA ANACONDA



Nyoka wa Anaconda hupatikana zaidi katika msitu wa Amazon
Watu nchini Marekani wameelezea ghadhabu na hasira zao kwenye mitandao ya kijamii kufuatia utafiti wa mtaalamu wa wanyamapori Paul Roslie kumezwa na Nyoka aina ya Anaconda ili ku chunguza maumbile ya ndani ya Nyoka huyo.
Lengo la utafiti huo ambao ulikuwa wa kwanza wa aina yake duniani, ilikuwa ni kuchunguza maumbulie ya ndani ya Nyoka huyo anayepatikana katika msitu wa Amazon.
Hata hivyo inaarifiwa bwana Paul alilazimika kusitisha utafiti wake ambao umezua utata muda mfupi tu baada ya kuuanzisha.
Watu nchini Marekani walijionea kwenye televisheni zao kipindi kilichokuwa kinapeperushwa cha mtaalamu huyo kuingia ndani ya tumbo la Anaconda akiwa amevalia vazi maalum ambalo yangesaidia kuchunguza kiwango cha joto mwilini mwake na pia kupima mipigo ya Moyo wake wakati akiwa ndani ya tumbo la Nyoka huyo.
Paul na vazi alilotumia kuingia ndani ya Nyoka kabla ya kushindwa na kusalimu amri
Rosolie na kikundi cha wasaidizi wake walipata Nyoka ya Anaconda mwenye uzito wa kilo 180, walipokuwa katika msitu huo. Alipanga kuwa ataonyeshwa kwenye stesheni hio akiwa anamezwa mzima mzima na Nyoka huyo.
Rosolie alionekana akiingia ndani ya mdomo wa Anaconda kwa kichwa chake huku wenzake wakimtazama.
Alikuwa amevalia vazi maalum lenye Carbon na likiwa limepakwa damu ya Nguruwe, kabla ya kujielkeza kwa Nyoka huyo kama mlo wake.
"sikutana kumhangaisha mno mnyama na pia mimi mwenyewe sikutaka kujiumiza. ''
Paul anapenda sana kujihusisha na maswala ya wanyama hasa Nyoka
"nilitaka kuhakikisha kuwa vazi langu halitamjeruhi Nyoka huyo kwa vyovyote vile.''
''Mimi mwenyewe sikuogopa hata kidogo. Watalaamu walifanyia jaribio vazi langu, kwa hivyo tulijua kuwa halitamwathiri kwa vyovyote Nyoka huyo. ''
Lakini baada tu ya saa moja ya mtaalamu kuingia ndani ya tumbo la Nyoka na kuanza kubanwa, aliamua kusitisha utafiti wake akihofia kuwa angeumizwa na Nyoka huyo mkubwa. Alisikika akiwaita wenzake kwa kifaa maalum cha kupaza sauti kilichokuwa kimewekwa kwenye vazi lake na kuwamabia kuwa anaumizwa.
''Nahisi kama mifupa yangu inasagwa sagwa, njooni mniondoe hapa.'' alisema Paul.
Namna ambavyo Rosolie aliponea kufa baada ya kubanwa na Nyoka huyo bado ni muujiza ingawa aliweza kupata hewa kutokaa kwa vazi lake hilo kwa saa tatu.
Imechapishwa na Unknown kwa 02:18
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Chapisho Jipya Taarifa za zamani Nyumbani
Jisajili kwenye: Chapisha Maoni (Atom)

Wachangiaji

  • Unknown
  • Unknown

Machapisho Maarufu

  • CHEKI WAREMBO WA KICHINA WAKIWA WAMEJIACHIA.....
  • MAJAMBAZI YAUWAWA KINYAMA HUKO KIGOMA...PICHA NI MBAYA SAMAHANI KWA HILO.
    Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa jeshi la polisi majambazi hayo yalikuwa yakikusudia kuteka magali huko Kasulu mko...
  • ANGALIA KATUNI MABALIMBALI ZA MASOOD KIPANYA.
  • SOMA HAPA UJUE ULE NINI KULINGANA NA KUNDI LA DAMU YAKO....
      Have you ever wondered why certain diets work for others and not for you, why you tend to gain weight even with a small helpings of your...
  • ZAIDI YA 52%YA WATANZANIA WATUMIA VIPODOZI VILIVYO PIGWA MARUFUKU..SOMA HABARI KAMILI HAPA!!
    Mamlaka ya chakula na dawa tanzania(TFDA) imesema watanzania takribani asilimia hamsini na mbili(52) wanawake kwa wanaume wako hata...
  • MWANGALIE PACHA WA MASOGANGE HAPA
           HUYO NDIYO LILY CORAZON MWENYE SHAPE KAMA YA AGNES MASOGANGE
  • MBASHA AKANA HANA MIMBA NA NGWAJIMA MIMBA NI YA MUMEWE MBASHA!
    Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Frora Mbasha amekana maneno yaliyo zagaaa mitaani kuwa mimba aliyo nayo ni ya Mbasha na si Ngwajima k...
  • HUYU NDIYO HAMISA MABETO ATUPIA PICHA YA NUSU UCHI INSTA.....MCHEKI HAPA!
  • Je wajua mnyama aliye hatarini kupotea?msome hapa...
                   Faru ndiye mnyama aliye hatarini kupotea duniani.
  • WAJUE WAIGIZAJI WATANO(5)WALIO KUFA WAKIWA WANAIGIZA.
       1.TYRON POWER   Alifariki kwa ugonjwa wa moyo mnamo March 15,1958,akiwa ndani ya chumba cha kuandalifilam.Tyron alikuwa maharufu s...

Kurasa

  • Nyumbani

Kumbukumbu la Blogu

  • ►  2015 (10)
    • ►  Machi (10)
  • ▼  2014 (144)
    • ▼  Desemba (2)
      • JAMAA MMOJA AFANYA UTAFITI NDANI YA TUMBO LA ANACONDA
      • MUUONE ZARI WA DIAMOND HAPA AKIWA KATIKA POZI MBAL...
    • ►  Oktoba (16)
    • ►  Septemba (80)
    • ►  Agosti (46)
Mandhari ya Dirisha la Picha. Inaendeshwa na Blogger.