
Mamlaka ya chakula na dawa tanzania(TFDA) imesema watanzania takribani asilimia hamsini na mbili(52) wanawake kwa wanaume wako hatarini kwa kupata madhara makubwa kama kansa ya ngozi,kuharibika kwa mimba na kujifungua watoto wenye ulemavu.
Hayo yamesemwa na mtoa mada na muelimishaji Bw. James Ndege.
imebainika kuwa idadi kubwa ya vipodozi hivyo ambavyo vimepigwa marufuku na mamlaka hiyo vimeingia ncnini kinyemela kwa njia za panya na wafanya biashsrs ambao si waadilifu na waaminifu.
Bw.Ndege ameongezea na kusema vipodozi hivyo ni hatari sana kwa matumizi ya binadamu kwani vina madini ya Zebaki na Hydroquinone na mengine mengi ambayo si rafiki kwenye mwili wa binadamu,hivyo amewataka watanzania kuwa makini na pia wasikimbilie vipodozi venye bei ndogo na kutoa rai kwa wafanya biashara hao kwani ulinzi umeimarishwa mipakani .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni