Alhamisi, 11 Septemba 2014

BUNGE LA KATIBA KUHAIRISWA,KATIBA YA SASA KUTUMIKA UCHAGUZI WA 2015.

Bunge maalum la katiba ambalo linaongozwa na Samweli Sitta akiwa ndiye mwenyekiti wa bunge hilo ambalo mbaka sasa limeshatumia zaidi ya Tsh.21 bill, linaelekea kuhairishwa kutokana na mambo mengi kutokamilika kwa kuto kukubaliana, huku Bunge la kaiwaida la Jamhuri likiwa lina karibia kuanza.
Bunge hilo ambalo lilikuwa na machafuko tangu mwanzoni mwa vikao juu ya posho na hata jinsi ya upigaji kura limeendelea kuwa na machafuko na hasa pale kikundi cha wapinzani hali maarufu UKAWA kuweka misimamo yao na hata kuwa nje ya bunge hilo.
Mbaka sasa hakijulikani hasa nini kinachoendelea kwenye bunge hilo ambalo limegharimu pesa nyingi za watanzania ambazo kama zinge wekwa kwenye huduma za jamii basi kuna hauweni ingeonekana.
Rais wa Tanzania Dr.Kikwete alijaribu kukutana na UKAWA na kukubaliana mambo kadha wa kadha na kupelekea bunge hilo kuhairishwa hadi hapo uchaguzi mkuu utakapo fanyika na kwamba katiba ya sasa ndiyo itakayo tumika kwa muda wote huo.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni