Bweni la wasichana katika shule ya sekondari African Muslim limeteketea kwa moto ,bweni hilo lenye vyumba 20 vya kulala wanafunzi hao wa kike limeungua vibaya kutokana na hitirafu ya umeme.
Shule hiyo iliyoko maeneo ya kata ya kaloleni,mkoani Kilimanjaro,yenye wanafunzi kuazia shule ya msingi hadi sekondari,wakiwa wamebakia wanafunzi wa madarasa ya mitihani tu yaani kidato cha nne,pili na darasa la saba ndipo bweni hilo linalotumiwa na wanafunzi wa kidato cha nne lilipo shika moto uliosemekana umetokea chooni na umesababishwa na hitirafu ya umeme na kutetekea.
Kwa taarifa tulizo zipokea hakuna mwanafunzi yeyote aliye poteza maisha katika ajali hiyo,zaidi ya wanafunzi kupotezea fahamu na baadae walipelekwa hospitari na kupata nafuu na kurudi shuleni.
mkurugezi wa shule hiyo Bw.ALI Adam Ali amesema hakukuwa na majanga makubwa na kuwa kuna baadhi ya wanafunzi waliweza kuokoa vitu vyao ikiwemo masanduku na magodoro japo kuna baadhi vitu vyao viliteketea,amesema anashukuru wanajamii wa kata hiyo kwani walijitokeza kusaidia kwenye tukio hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni