Ijumaa, 12 Septemba 2014

DAKTARI ALIYEUGUA EBOLA SASA KUREJEA AFRICA BAADA YA KUPONA

Muingereza huyo Wiliam Pooley ambaye aliambukizwa ugonjwa wa ebola akiwa Africa anasema anataka kurejea Siera Leone huku akiya sihi mataifa makubwa ya mang'aribi kuongeza bidii katika kupambana na ugonjwa huo hatari.
Wiliam Pooley anawasihi viongozi wakubwa kuonesha uongozi wao katika kupambana na ugonjwa huo akisema "ni tatizo kubwa la dunia,na inawahitaji viongozi wakubwa wa dunia..hivyo Obama na Cameron wanahitajika kuonesha uongozi katika swala hili"
Wiliam Pooley alipona ugonjwa wa ebola baada ya kupokea huduma ya hali ya juu kutoka hospitali ya Royal Free ya jini London

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni