Jumanne, 2 Septemba 2014

WAFANYA BIASHARA WAKINUKISHA KARIAKOO,NI KUHUSU MASHINE ZA EFD

Wafanya biashara wa mjini Kariakoo  jijini Daresalaam,wamefunga maduka yao wakipinga matumizi ya mashine za kutunza rekodi na kutoa risiti kwa wateja kwa lengo la kukusanya mapato kikamilifu zoezi linalo endeshwa na TRA.
Wafanya biashara hao wakiongea kwa nyakati tofauti wamesema wamefunga maduka hayo si kwakuwa hawazitaki mashine hizo bali gharama za mashine hizo ziko juu sana na pia wanahitajika kuzifanyia matengenezo pindi ziaribikapo kwa gharama zao.
Wakiongea kwa hisia na machungu wanasema hawajui hatima yao kwani kwao biashara ndio hajira  na ndio muhimili wa familia zao.
Mama Sakina na mzee Masawe wanasema wana watoto wanasomesha kwa kupitia sikoni hapo na pia wanamajukumu mengine ya kifamilia na kijamii sasa TRA wanapowalazimisha wanunue mashine hizo kwa gharama kubwa hivyo wanawaumiza ki maslai.


Maduka mengi ya sokoni hapo yamefungwa na hata wale wenye mashine pia wamefunga maduka yao wakihofia kuvamiwa na wafanya biashara wenzao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni