Kwa mujibu wa Cheyo ambaye ndiye kiongozi wa TCD amesema mkutano umekwenda vizuri na kubwa walilokuwa wakizungumzia ni namna ya kukamilisha katiba mpya pamoja na uchaguzi ujao wa mwaka 2015.
TCD ikiongozwa na mwenyekiti wa UDP Bwana John Cheyo inamatumaini na mkutano huo kwa yale walio kubaliana na Rais Kikwete na kuongeza pia hakukuwa na fujo zozote ndani ya ukumbi na badala yake wamekubaliana kuonana tena na Rais tarehe 8,mwenzi huu wa tisa.
Kwenye mkutano huo kulikuwa na wenye viti na makatibu wa vyama vinavyo unda TCD,alikuwemo Mh.Mrema,Mbunge wa Vunjo,DR.Slaa ,Katibu wa CHADEMA,pamoja na Lisu Mwanasheria wa CHADEMA,Mh.James Mbatia ,Mwenyekiti NCCR Mageuzi na Mwenyekiti wa CUF Bw.Ibrahim Lipumba na wengineo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni