Japokuwa
Urusi inaaminika kuwa na silaha nyingi hatari za kivita lakini mtandao
wetu kwa msaada wa mtandao wa yahoo.com unakuletea ndege ambazo ni
hatari zaidi zinaposhambulia toka angani zinazomilikiwa na Urusi.
1.PAK FA
PAK FA.
PAK
FA ina rada maalum ya kivita inayosaidia kutazama muelekeo na
kuchunguza umbali mrefu kabla ya kufika eneo husika, licha ya uwezo wa
kubeba silaha nyingine pia ina uwezo wa kubeba makombora makubwa sita
ikiwa ni pamoja na kutupa toka hewani pamoja na ardhini.
PAK
kwa mara iliruka hewani kwa dakika 47 January 29, 2010 na baada ya hapo
ilifanyiwa majaribio zaidi ya 450 mwishoni mwa mwaka 2013.
Russia
inatarajia kutengeneza ndege kama hizo 400 mpaka 450 kufikia mwaka 2020
au 20140 katika mradi ambao inashirikiana na India iliyochangia kiasi
cha dola bilioni 6 ili kufanikisha mpango huo.
2.Su-25 FROGFOOT
Su-25 FROGFOOT. Picha|digitalcombatsimulator.
Ndege
hii ina kasi sana na ina sehemu kumi ambazo zinawekwa mabomu ili
kushambulia, pia ina uwezo wa kushambulia hewani kwa hewani ikiwa na
maana kutungua ndege nyingine hewani na pia kushambulia toka hewani
kwenda ardhini.
Ndege hii ilitengenezwa maalum kushambulia ikiwa karibu na uwanja wa vita si kutoka mbali pia inabeba makombora.
Ndege hii imeshawahi kushambulia Afghanistan mwaka 1979-1989, vita ya Chechnya na sasa hivi inatumika katika mgogoro wa Ukraine.
3.Tu-95 BEAR STRATEGIC BOMBER
Ndege
hii ilitengenezwa maalum kwa kurusha mabomu ya nyuklia lakini imekuwa
ni vigumu kwa mabomu hayo kutumika kutokana na mpango wa Marekani wa
kupinga matumizi ya mabomu hayo hatari Duniani.
Kutokana
na kasi yake, ndege hii ilitumika kwenye vita ya baridi kufanya doria
kaskazini mwa bahari ya Atlantic pamoja na kuongoza vikosi vya majeshi
ya maji.
Ndege hii kwa sasa ipo katika matengenezo ya kuiboresha zaidi kwa sababu ilitengenezwa miaka 60 iliyopita.
4.Tu-160 BLACKJACK STRATEGIC BOMBER
Ndege
hii ilikuwa ni toleo la mwisho mwaka 1980-1992 la Soviet Union kabla
haijasambaratika na Russia kumiliki zana nyingi za kivita.
Ndege
hii ina uwezo mkubwa wa kufanya shughuli za kivita usiku katika hali
zote za hewa huku ikiwa imebeba mzigo mkubwa wa mabomu ya nyuklia pamoja
na makombora yenye uzito mkubwa.
Ndege hii ina kasi ya kilomita 2,000 kwa saa pamoja na kutembea umbali wa kilomita 14,000 bila kujazwa mafuta kwa mara nyingine.
Ndege hii pia kutokana na muundo wake ina uwezo wa kugundua kombora lililoelekezwa kwake na kukwepa kabla halijaleta madhara.
5.Su-35 FLANKER FIGHTER
Su-35 FLAKER FIGHTER. Picha presstv.ir.
Ndege hii ina kifaa maalum kinachoweza kumtafuta adui umbali wa kilomita 400 na kumshambulia.
Ndege
hii ambayo ina injini mbili pia ina uwezo wa kubeba mzigo mkubwa wa
silaha mbalimbali pamoja na maeneo 14 yanayofungwa silaha kwa ajili ya
kushambulia.
*Mpangilio wa namba haumaanishi kuwa iliyo namba moja ndio inaongoza au namba tano ndio ya mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni