MOHAMED BADIE
Mahakama nchini Misri imemhukumu kiongozi wa
kidini wa kundi la Muslim Brotherhood,Mohamed Badie kifungo cha maisha
jela,yeye pamoja na wafuasi wake wapatao kumi na wanne.
Badie
amehukumiwa kufuatia kukutwa na hatia ya makosa ya mauaji na ukatili na
pia kutaka kumng'oa madarakani rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi mnamo
mwaka 2013,Badie tayari ameanza kutumikia kifungo hicho .Hata hivyo mwanaharakati mashuhuri Alaa Abdel-Fattah yeye ameachiliwa huru katika mahakama ingine,Alaa alihukumiwa miaka 15 jela kwa kushiriki katika maandamano ambayo yalizuiliwa mnamo mwaka wa jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni