Siku
moja baada ya makamu wa rais dkt mohamed ghalib bila kuhimiza mahusiano
mema wakati wa utendaji kazi baina ya vyombo vya ulinzi na usalama na
vyombo vya habari jeshi la polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa
limekiuka kauli hiyo kwa kuwapiga na kuwajeruhi baadhi ya waandishi wa
habari na kuwazuia kutekeleza wajibu wao wakati mwenyekiti wa Chama cha
demokrasia na maendeleo Chadema alipowasili katika makao makuu ya jeshi
hilo kwa mahojiano.
Kauli hiyo ya makamu wa rais imeshindwa kutekelezwa
kutokana na tukio lililotokea majira ya saa 5 na dk 15 asubuhi wàkati
mwenyekiti wa chadema taifa Mhe. Freeman Mbowe alipowasili makao makuu
na askari wa polisi kutaka kuzuia gari alilopanda kuingia ndani ya
lango kuu pamoja na waandishi wa habari na watu wengine kuamriwa
kuondoka katika eneo hilo agizo lililopingwa na waandishi wa habari na
baadhi ya wanasheria wa Chadema.
Kufuatia na kutolewa kwa ilani hiyo jeshi la polisi
kikosi cha kutuliza ghasia-FFU- kilianza kupiga waandishi wa habari
pamoja na baadhi ya wananchi huku wengine wakikimbia kuhofu vipigo toka
kwa askari hao ambapo baaadhi ya waandishi walioumizwa sehemu mbalimbali
ya mihili yao.
Akiwatangazia wafuasi waliokuwa wakikataa kuondoka
katika maeneo hayo mwanasheria wa chadema mhe. Tundu lissu licha ya
kuwahakikishia kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa Mhe. Freeman Mbowe
yuko salama amewataka kuondoka katika eneo hilo na kurudi majumbani ili
kuepusha vurugu na misongamano ambayo ingeweza kusababisha matatizo
zaidi.
Aidha ITV imeshuhudia mwenyekiti wa Chadema taifa
Mhe Freeman Mbowe akitoka makao makuu ya jeshi la polisi akisindikizwa
na ulizni mkali wa jeshi la polisi kuelekea katika ofisi za makao makuu
ya chama hicho baada ya kukamilika kwa taratibu za kipolisi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni