
Idadi ya watu waliokufa kwenyeghorofa la makao makuu ya Kanisa la SCOAN
(Synagogue Church of All Nations) la Nabii TB Joshua wamefikia 50.Jengo
hilo la ghorofa tano ambalo ni makao makuu ya kanisa na nyumba ya kulala
wageni liliporomoka Jumamosiwakati ujenzi ukiendelea.Hadi kufikia jana
Jumapili jumla ya watu 41 walikuwa wameripotiwa kufa, lakini
maitinyingine tisa zimeongezeka leo hii.Inaelezwa kwamba, mhubirihuyo wa
kimataifa alipewa kibali cha kujenga ghorofa mbili, lakini mwenyewe
akaamua kujenga ghorofa tano.Uokoaji bado unaendelea na watu wengine 124
walikuwa wameokolewa wakiwa hai hadi kufikia jana Jumapili.
Mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kanisa hilo akiwa
hajitambui.Jengo hilo liko katika eneo la Ikotun magharibi mwa Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Lagos.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni