THE EVENT

Jumanne, 9 Desemba 2014

JAMAA MMOJA AFANYA UTAFITI NDANI YA TUMBO LA ANACONDA



Nyoka wa Anaconda hupatikana zaidi katika msitu wa Amazon
Watu nchini Marekani wameelezea ghadhabu na hasira zao kwenye mitandao ya kijamii kufuatia utafiti wa mtaalamu wa wanyamapori Paul Roslie kumezwa na Nyoka aina ya Anaconda ili ku chunguza maumbile ya ndani ya Nyoka huyo.
Lengo la utafiti huo ambao ulikuwa wa kwanza wa aina yake duniani, ilikuwa ni kuchunguza maumbulie ya ndani ya Nyoka huyo anayepatikana katika msitu wa Amazon.
Hata hivyo inaarifiwa bwana Paul alilazimika kusitisha utafiti wake ambao umezua utata muda mfupi tu baada ya kuuanzisha.
Watu nchini Marekani walijionea kwenye televisheni zao kipindi kilichokuwa kinapeperushwa cha mtaalamu huyo kuingia ndani ya tumbo la Anaconda akiwa amevalia vazi maalum ambalo yangesaidia kuchunguza kiwango cha joto mwilini mwake na pia kupima mipigo ya Moyo wake wakati akiwa ndani ya tumbo la Nyoka huyo.
Paul na vazi alilotumia kuingia ndani ya Nyoka kabla ya kushindwa na kusalimu amri
Rosolie na kikundi cha wasaidizi wake walipata Nyoka ya Anaconda mwenye uzito wa kilo 180, walipokuwa katika msitu huo. Alipanga kuwa ataonyeshwa kwenye stesheni hio akiwa anamezwa mzima mzima na Nyoka huyo.
Rosolie alionekana akiingia ndani ya mdomo wa Anaconda kwa kichwa chake huku wenzake wakimtazama.
Alikuwa amevalia vazi maalum lenye Carbon na likiwa limepakwa damu ya Nguruwe, kabla ya kujielkeza kwa Nyoka huyo kama mlo wake.
"sikutana kumhangaisha mno mnyama na pia mimi mwenyewe sikutaka kujiumiza. ''
Paul anapenda sana kujihusisha na maswala ya wanyama hasa Nyoka
"nilitaka kuhakikisha kuwa vazi langu halitamjeruhi Nyoka huyo kwa vyovyote vile.''
''Mimi mwenyewe sikuogopa hata kidogo. Watalaamu walifanyia jaribio vazi langu, kwa hivyo tulijua kuwa halitamwathiri kwa vyovyote Nyoka huyo. ''
Lakini baada tu ya saa moja ya mtaalamu kuingia ndani ya tumbo la Nyoka na kuanza kubanwa, aliamua kusitisha utafiti wake akihofia kuwa angeumizwa na Nyoka huyo mkubwa. Alisikika akiwaita wenzake kwa kifaa maalum cha kupaza sauti kilichokuwa kimewekwa kwenye vazi lake na kuwamabia kuwa anaumizwa.
''Nahisi kama mifupa yangu inasagwa sagwa, njooni mniondoe hapa.'' alisema Paul.
Namna ambavyo Rosolie aliponea kufa baada ya kubanwa na Nyoka huyo bado ni muujiza ingawa aliweza kupata hewa kutokaa kwa vazi lake hilo kwa saa tatu.
Imechapishwa na Unknown kwa 02:18 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

MUUONE ZARI WA DIAMOND HAPA AKIWA KATIKA POZI MBALIMBALI



GAZETI GANI?
Gazeti la Red Pepper la Desemba 5, mwaka huu ndilo lililomponza mwanadada huyo kwa kuripoti kuvuja kwa video ya utupu ya mrembo huyo na kusababisha aonekane hafai mbele ya jamii. Wadau wengi wakaanza kuhoji kwa nini akubali kurekodiwa video hiyo wakati yeye ni mtu mzima tena mama wa watoto watatu?
VIDEO YAZUA GUMZO
Vyanzo tofauti mitandaoni vimeielezea video hiyo. Kuna ambavyo vimedai kuwa mwanadada huyo alirekodiwa ‘akijichua’ mwenyewe huku vyanzo vingine vikienda mbali zaidi kwa kudai alirekodiwa akivunja amri ya sita na mpenzi wake wa zamani.
ZARI AFUNGUKA
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari mwenye maskani yake nchini Uganda na Afrika Kusini, aliandika kuwa mtu aliyevujisha video hiyo chafu alikuwa na lengo la kumharibia shoo yake anayotarajia kuifanya Desemba 18, mwaka huu inayofahamika kama Zari All White Party lakini hawatafanikiwa. 
Zari, ‘The Boss Lady’ akipozi.
“Hii ni kwa mashabiki wangu wote duniani, vyombo vya habari vya Uganda vimenichafua kwa kuingilia uhuru wangu pamoja na familia yangu ili kuniharibia na picha hizi za zamani... katika akili yangu najua kabisa picha zilizotoka leo (Ijumaa iliyopita) kwenye Gazeti la Red Pepper zimevujishwa na mtu kwa madhumuni yake binafsi.
“Kimsingi sitashindwa, shoo itafanyika kama kawaida na Diamond atakuwepo kama kawaida. Niwahakikishie tu nitachukua hatua za kisheria kwa yeyote aliyehusika kunichafua,” aliweka nukta Zari.
GAZETI LAKOMAA
Licha ya mwanadada huyo kudai atawafikisha kwenye mikono ya sheria wahusika wote, bado ilielezwa kuwa gazeti hilo lilizidi kukomaa na kudai wana ushahidi wa kutosha.
 
Zari, ‘The Boss Lady’ akila ujana.
WABONGO SASA
Mara baada ya habari hiyo kuzagaa mitandaoni, Wabongo walilipuka kama moto wa kifuu na kuanza kutoa maoni kuhusu mrembo huyo ambapo wengi walidai ni mara mia Diamond angeendelea kuwa na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ‘Madam’ kuliko Zari.
“Mmeona sasa mtu ambaye Diamond aliona amepata kumbe si lolote si chochote, mtu mwenye akili zake atakubalije kurekodiwa video ya utupu? Kwa kweli mara mia Diamond angebaki na Wema wake ambaye hana skendo kubwa kama hii, Zari kwisha kabisa, hapa ndiyo mwisho wake, aibu ya mwaka hii,” alichangia mdau mmoja mtandaoni.
MWINGINE AMTETEA
Pamoja na wadau wengi kumponda Zari na kudai ndiyo mwisho wa heshima yake, kuna mdau mwingine mtandaoni alimtetea mrembo huyo anayefanya muziki kuwa ni mwanamke jasiri na Diamond anatakiwa kuwa pamoja naye kuhakikisha wanaizima skendo hiyo, waendelee kufanya yao.
“Kiukweli nimempenda Zari, anajiamini hakuona umuhimu wa kuomba radhi maana anajua ni vitu ambavyo alivifanya kabla hajakutana na Diamond,” alichangia mdau mmoja mtandaoni.
Zari, ‘The Boss Lady’ akiwa na 'Diamond'.
TIMU WEMA VICHEKO
Wakati saga hilo likizidi kupata ‘kavareji’ mitandaoni, wafuasi wa Wema (Timu Wema) waliashiria kufurahia kitendo cha mrembo huyo kurekodiwa video hiyo ya utupu.

“Safii, si alijifanya anajua kutuchukulia shemeji letu sasa limemshuka shuuu...akome,” mmoja wa memba wa Timu Wema alitupia komenti yake.
HATA HIVYO
Hata hivyo, ikumbukwe kwamba, Wema ndiyo alimmwaga Diamond na si Diamond kummwaga Wema wala kumwagana!
TUJIKUMBUSHE!
Zari na Diamond wanaodaiwa kuzalisha penzi jipya hivi karibuni (project), kila kukicha wamekuwa wakinadi urafiki wao mitandaoni huku kila mmoja akionesha kumsapoti mwenzake kimuziki ambapo Desemba 18, mwaka huu wameahidi kufanya bonge la shoo nchini Uganda.

Pichani ‘Zari’, ‘The Boss Lady’ akiwa mtupu.
K
Imechapishwa na Unknown kwa 02:16 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

Alhamisi, 30 Oktoba 2014

SRI LANKA YAPATA MAAFA YA MMOMONYOKO WA ARDHI..

Inaelezwa kuwa baada ya mvua kubwa iliyopelekea udongo uporomoka na kusababisha maafa makubwa huko Nchini Sri Lanka inakadiriwa idadi kubwa ya watu watakuwa wamepoteza maisha na wengine wasijue hatima ya maisha yao kwakuwa hakuna kilicho salia,si nyumba wala mifugo hata mazao pia vyote vimeadhiriwa vibaya.




Embedded image permalink







Imechapishwa na Unknown kwa 01:25 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

HAYA NDIYO MAGAZETI YA LEO TAREHE 30.0CT.2014


.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
..
..
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Image00045
.
.
.
.
.
.
.
.
Image00005
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Imechapishwa na Unknown kwa 01:08 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

Alhamisi, 16 Oktoba 2014

TOYOTA KUCHEKI ZAIDI YA MAGARI 1.67 MIL DUNIANI KOTE

KampunikkkEmbedded image permalink
Imechapishwa na Unknown kwa 00:44 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

ZIMBABWE WAGUNDUA KAHAWA INAYO ZIDISHA NGUVU ZA KUFANYA TENDO LA NDOA.





Maporomoko ya maji ya Zimbabwe

Ama kwa hakika duniani kuna mambo! wachuuzi wa kahawa yenye vijimambo ndani yake,ambayo ukiinywa tu basi inakupa mzuka wa kufanya ngono kwa kiwango cha hali ya juu na biashara inawaendea vyema katika mitaa ya Harare nchini Zimbabwe.
Kahawa hiyo huuzwa kati ya dola za kimarekani 3 hadi 5 kwa kifuko kidogo kinachotosha kikombe kimoja cha chai, na bei hiyo itategemea jinsi wewe ulivyo mtaalamu wa kuomba punguzo la bei inaweza kushuka .
Wachuuzi hao wa mitaa ya Harare wamezungumza na kudai kuwa kahawa hiyo huwasaidia wanaume kupata hamu ya kufanya ngono kwa muda mrefu Zaidi,lakini pia humchelewesha mwanaume kupata mshindo kwa muujibu wa utafiti wao.
Pindi tu uinunuapo kahawa hiyo,wachuuzi hao hukupa maelekezo kuwa uinywe dakika 15 kabla ya tukio lenyewe na humpa nguvu mtumiaji ya kufanya ngono kwa saa sabini na mbili,ingawa madai hayo hayajathibitishwa kitabibu.
Wachuuzi hao wameamua kufanya biashara yao katika mtindo wa aina yake,kwa kuiuza kahawa hiyo katika maeneo maarufu nchini Zimbabwe yenye mikusanyiko ya watu kama eneo la KwaMereki kwenye viunga vya bustani ya kitongoji cha Warren, Zindoga eneo lililoko kwenye maporomoko ya maji (Waterfalls) na eneo la vilima la KuHuku .
Kitu cha kuvutia biashara hiyo hufanywa na wachuuzi wa kike wafanyao kazi katika duka kubwa la Fife Avenue Shopping centre wenye kutoa ushuhuda na kukubali kuwa waume zao waliitumia kahawa hiyo na wakayaona matokeo yake nao wakafaidi kwani uwezo wao uliongezeka maradufu.
Ingawa wanawake hao pamoja na kukubali na kutoa ushuhuda huo, bado hawako tayari kuelezea wapi wanakozinunua kahawa hizo za majamboz na kwasasa mjini Harare mahitaji ya kahawa hiyo ni makubwa mno na ni rahisi kuitumia kwani unaweza kuitumia kwa maji moto ama baridi anaeleza muuzaji aliyejitaja kwa jina moja la Anna.
Anna anasema wateja wake wakubwa ni waume kwa wake ingawa wanawake wana aibu kuinunua kahawa hiyo hadharani kuliko wanaume wao hawana aibu pindi wanapotaka kahawa hiyo kwa matokeo mazuri ya kulinda heshima shughulini.
Kwa muujibu wa daktari mmoja nchini Zimbabwe aliyekataa kutajwa jina lake amesema kwamba tatizo la nguvu za kiume nchini Zimbabwe ni kubwa mno kwa wanaume walio wengi na linakua siku hadi siku na kusema ni tatizo kubwa.
Imechapishwa na Unknown kwa 00:36 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest
Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Nyumbani
Jisajili kwenye: Machapisho (Atom)

Wachangiaji

  • Unknown
  • Unknown

Machapisho Maarufu

  • CHEKI WAREMBO WA KICHINA WAKIWA WAMEJIACHIA.....
  • MAJAMBAZI YAUWAWA KINYAMA HUKO KIGOMA...PICHA NI MBAYA SAMAHANI KWA HILO.
    Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa jeshi la polisi majambazi hayo yalikuwa yakikusudia kuteka magali huko Kasulu mko...
  • ANGALIA KATUNI MABALIMBALI ZA MASOOD KIPANYA.
  • SOMA HAPA UJUE ULE NINI KULINGANA NA KUNDI LA DAMU YAKO....
      Have you ever wondered why certain diets work for others and not for you, why you tend to gain weight even with a small helpings of your...
  • ZAIDI YA 52%YA WATANZANIA WATUMIA VIPODOZI VILIVYO PIGWA MARUFUKU..SOMA HABARI KAMILI HAPA!!
    Mamlaka ya chakula na dawa tanzania(TFDA) imesema watanzania takribani asilimia hamsini na mbili(52) wanawake kwa wanaume wako hata...
  • MWANGALIE PACHA WA MASOGANGE HAPA
           HUYO NDIYO LILY CORAZON MWENYE SHAPE KAMA YA AGNES MASOGANGE
  • MBASHA AKANA HANA MIMBA NA NGWAJIMA MIMBA NI YA MUMEWE MBASHA!
    Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Frora Mbasha amekana maneno yaliyo zagaaa mitaani kuwa mimba aliyo nayo ni ya Mbasha na si Ngwajima k...
  • HUYU NDIYO HAMISA MABETO ATUPIA PICHA YA NUSU UCHI INSTA.....MCHEKI HAPA!
  • Je wajua mnyama aliye hatarini kupotea?msome hapa...
                   Faru ndiye mnyama aliye hatarini kupotea duniani.
  • WAJUE WAIGIZAJI WATANO(5)WALIO KUFA WAKIWA WANAIGIZA.
       1.TYRON POWER   Alifariki kwa ugonjwa wa moyo mnamo March 15,1958,akiwa ndani ya chumba cha kuandalifilam.Tyron alikuwa maharufu s...

Kurasa

  • Nyumbani

Kumbukumbu la Blogu

  • ►  2015 (10)
    • ►  Machi (10)
  • ▼  2014 (144)
    • ▼  Desemba (2)
      • JAMAA MMOJA AFANYA UTAFITI NDANI YA TUMBO LA ANACONDA
      • MUUONE ZARI WA DIAMOND HAPA AKIWA KATIKA POZI MBAL...
    • ►  Oktoba (16)
      • SRI LANKA YAPATA MAAFA YA MMOMONYOKO WA ARDHI..
      • HAYA NDIYO MAGAZETI YA LEO TAREHE 30.0CT.2014
      • TOYOTA KUCHEKI ZAIDI YA MAGARI 1.67 MIL DUNIANI KOTE
      • ZIMBABWE WAGUNDUA KAHAWA INAYO ZIDISHA NGUVU ZA KU...
    • ►  Septemba (80)
    • ►  Agosti (46)
Mandhari ya Dirisha la Picha. Inaendeshwa na Blogger.