Familia ya Baba wa Taifa waiomba benki kuu ya Tanzania kuondoa noti ya shilingi elfu moja.

Familia
ya baba wa taifa hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere imeuomba
uongozi wa benki kuu ya Tanzania kuiondoa katika mzunguko wa fedha noti
ya shilingi elfu moja yenye picha ya Baba kwa maelezo kuwa picha ambayo
imetumika katika noti hiyo haifanani kabisha na kiongozi huyo na kwamba
kuendelea kutumika ni sawa na kumdhalilisha muasisi huyo wa taifa la
Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya familia na ukoo wa Baba wa taifa wakati wa
kupokea mradi wa kuboresha makumbusha ya Mwalimu Nyerere na kuzindua
onesho la noti na sarafu ambazo zimetumika katika vipindi tofauti
kuanzia mwaka 1967 hadi sasa zenye picha na sahihi ya Baba wa taifa,
mmoja wa watoto wa Baba wa taifa Bw Madaraka Nyerere, amesema picha
iliyopo katika noti hiyo ya shilingi elfu moja haifanani na sura ya
kiongozi huyo hivyo kuomba benki hiyo kuangalia uwezekano wa kuiondoka
katika mzunguko.
Naye kaimu gavana wa benki kuu ya Tanzania Bw Juma Reli, pamoja na
kutoa ahadi ya ukarabati nyumba ya kwanza ya Baba wa taifa ambayo
aliitumia kabla ya kujengewa na tanu amesema kuwa benki hiyo imejitolea
kuboresha makumbusho hayo ili kuhifadhia kumbukumbu zenye histori ya
baba wa taifa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wao mkurugenzi mkuu wa shirika la makumbusho ya taifa
Profesa Audax Mabula na mkuu wa wilaya ya butiama Bi Angelina Mabula,
wameishukuru benki kuu ya Tanzania kwa kutambua umuhimu wa kuboresha
makumbusho hayo katika kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali za Baba wa taifa
Mwalimu Julius Nyerere ili kulinda historia za kiongozi huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni