
Katika
hali isiyo ya kawaida mechi kati ya Serbia na Albania imeshindwa
kumalizika baada ya ndege isiyokuwa na rubani kubeba ujumbe wa kisiasa
kusababisha vurugu zilizowahusisha wachezaji na mashabiki ndani ya
uwanja wa Partizan.
Mechi
hiyo ya kufuzu katika michuano ya soka bara la Ulaya mwaka 2016
ilisimamishwa na mwamuzi Martin Atkinson kutoka Uingereza katika dakika
ya 41 ya mchezo huo huku matokeo yakisomeka 0-0.
Vurugu
ziliibuka wakati bendera ya Albania na ujumbe kupeperushwa juu ya
uwanja na kushikwa na wachezaji wa Serbia. Wachezaji wa Serbia
walijaribu kuichukua bendera hiyo mbele ya mashabiki kadhaa ilichanika
ndani ya uwanja.
'Tukio
moja la kijinga limesababisha vurugu- hiyo ndio njia ya mkato
kulielezea tukio lililotokea usiku' alisema mwandishi wa televisheni ya
B92 Milos Saranovic.
Mwamuzi
Atkinson aliwaondoa wachezaji nje ya uwanja na baada ya kuchelewa kwa
dakika 30 Uefa ilithibitisha kusitishwa kwa mchezo huo.
Serbia
na Albania wanahistoria ya kutoelewana mara kwa mara ikihusishwa na
jimbo la zamani la Serbia Kosovo jimbo ambalo lilijipatia uhuru mwaka
2008.
M
A
L
U
N
D
E
1
B
L
O
G
,
F
A
H
A
R
I
Y
A
S
H
I
N
Y
A
N
G
A
!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni