Alhamisi, 16 Oktoba 2014

IDADI YA VIFO VYA AJALI YA MLIPUKO WA PETROL ULIOTOKEA MBAGALA YAONGEZEKA

Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa ajali ya moto uliosababishwa na watu waliokuwa wakiiba mafuta ya petroli baada lori lililobeba shehena ya mafuta hayo kuanguka karibu na makazi ya watu eneo la mbagala Charambe jiji Dar es Salaam imeongezeka na kufikiwa watano.
Akizungumza na waandishi wa habari afisa uhusiano wa hospiatli ya taifa ya Muhimbili, Bi Doris Ishinda amesema vifo vya wagonjwa wawili zaidi vimeongezeka jana jioni na usiku wa kuamkia leo na kufanya idadi ya wagonjwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili mpaka sasa kuwa kumi na moja.
 
Aidha katika hospitali ya Temeke wagonjwa wanne wanaendelea kupata matibabu na kufanya idadi ya wagonjwa waliolazwa mpaka sasa kupungua hadi kufikia 15 katika hospitali ya Temeke na Muhimbli na vifo imeongezeka toka vifo vitatu hadi vitano.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni