Jumatatu, 25 Agosti 2014

......."NI KISASI'...........

London, England. Mechi kubwa ya wiki ya Ligi Kuu England itachezwa leo usiku kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester. Mechi hiyo itaikutanisha Manchester City dhidi ya Liverpool leo saa nne usiku. Timu hizi zilimaliza msimu uliopita zikiwa katika nafasi mbili za juu katika Ligi Kuu England. Manchester City ilishika nafasi ya kwanza huku Liverpool ikiwa nafasi ya pili. Katika msimu huu timu hizi zimeanza vizuri ligi hiyo kwani Liverpool inayonolewa na kocha Brendan Rodgers iliibuka na ushindi wa mabao 2 -1 dhidi ya Southampton, pia City iliyo chini ya kocha Manuel Pellegrini waliianza ligi hiyo kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle. Itakumbukwa kwamba mara ya mwisho timu hizi kukutana katika ligi kuu ya premier ilikua pale anfield ambapo Man city walilala kwa mabao 3 kwa 2...swali kubwa ni "je Man City wataweza kulipa kisasi"? “Hii ni mechi muhimu, timu hizi mbili zilifanya vizuri katika msimu uliopita wa Ligi Kuu England,”alisema Rodgers. Naye kocha Pellegrini alisema,”Nafikiri tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii, hatutakiwi kuruhusu mabao, pia tunatakiwa kujiamini zaidi kwani tuna kikosi bora.” Katika mechi 10 zilizopita zilizozikutanisha timu hizi, Man City ilishinda tatu kwenye Uwanja wa Etihad wakati Liverpool ilishinda mbili Anfield. Pia zilitoka sare tano, ambapo mbili uwanja wa Etihad na tatu kwenye Uwanja wa Anfield.

Maoni 1 :