Jumamosi, 27 Septemba 2014

JEREMY MATHIEU NA DANI ALVES WARUDI KIKOSINI TAYARI KWA KAZI...

HADI HALF -TIME LIVERPOOL0 -0EVERTON

 

SOMA HAPA UJUE ULE NINI KULINGANA NA KUNDI LA DAMU YAKO....

 
Have you ever wondered why certain diets work for others and not for you, why you tend to gain weight even with a small helpings of your favorite dish but others don’t. :(( Few months back, I read an article in Times of India regarding ‘Blood Group Diet’, its efficiency, how can we prevent occurrence of various diseases and increase our lifespan. So I thought, why not to share something beneficial with you all? :))
Blood Group Diet is a concept introduced by Dr Peter J D Adamo, author of “Eat right for your Type.” This diet propagates that our blood group determines how our bodies deal with different nutrients. It is based on the ideology that each blood group has its own antigen markers and these markers have different responses with food components. Consequently a diet designed specifically for your blood type allows your body to digest and absorb food more efficiently, with the result that you lose weight. It groups people into:
- High protein/ Meat eaters (Type O)
-Vegetarians (Type A)
– Balanced omnivore (Type B)
– Mixed diet moderation (Type AB).

According to Dr. Peter J D Ádamo, author of Eat Right For Your Type, a chemical reaction occurs between your blood and the foods you eat. This reaction is part of your genetic inheritance. This reaction is caused by a factor called Lectins. Lectins, abundant and diverse proteins found in foods, have agglutinating properties that affect your blood. So when you eat a food containing protein lectins that are incompatible with your blood type antigen, the Lectins target an organ or bodily system and begin to agglutinate blood cells in that area.
Fortunately, most lectins found in the diet are not quite so life threatening, although they can cause a variety of other problems, especially if they are specific to a particular blood type. For the most part your immune systems protect you from lectins. Ninety-five percent of the lectins you absorb from your typical diets are sloughed off by the body. But at least five percent of the lectins you eat are filtered into the bloodstream and different reactions occur in different organs.
Your blood type diet is the restoration of your natural genetic rhythm. Your blood type diet works because you are able to follow a clear, logical, scientifically researched plan based on your cellular profile. Each food groups are divided into three categories:
-Highly beneficial (food that acts like Medicine)
-Foods allowed (food that are no harm to the blood type)
-Foods not allowed (food that acts like a Poison)


Blood Type Diet – Type O

-Type Os thrive on intense physical exercise and animal protein. Unlike the other blood types, Type Os muscle tissue should be slightly on the acid side. Type Os can efficiently digest and metabolize meat because they tend to have high stomach-acid content. The success of the Type O Diet depends on the use of lean, chemical-free meats, poultry, and fish. Type Os don’t find dairy products and grains quite as user friendly as do most of the other blood types.
-The initial weight loss on the Type O Diet is by restricting consumption of grains, breads, legumes, and beans.
-The leading factor in weight gain for Type Os is the gluten found in wheat germ and whole wheat products, which interferes with insulin efficiency and slow down metabolic rate.
-Another factor that contribute to weight gain is certain beans and legumes (lentils and kidney beans) contain lectins that deposit in the muscle tissues making them less “charged” for physical activity.
-The third factor in Type O weight gain is that Type Os have a tendency to have low levels of thyroid hormone or unstable thyroid functions, which also cause metabolic problems.
-Therefore it is good to avoid food that inhibits thyroid hormone (cabbage, brussels sprouts, cauliflower, mustard green) but increase hormone production (kelp, seafood, iodized salt).
-Several classes of vegetables can cause big problems for Type Os, such as the Brassica family (cabbage, cauliflower, etc.) can inhibit the thyroid function. Eat more vegetables that are high in Vitamin K, which helps the clotting factor which is weak in Type Os. The nightshade vegetables can cause lectin deposit in the tissue surrounding the joints.
-Because of the high acidity stomach, Type Os should eat fruits of alkaline nature such as berries and plums..
-Type Os should severely restrict the use of dairy products. Their system is not designed for the proper metabolism. If you are a Type O of African ancestry, you should eliminate dairy foods and eggs altogether.

Blood Type Diet – Type A

My blood group is Type A, I am not fond of meat much but I love mangoes and that is not allowed for my blood type. :(
– Type As flourish on vegetarian diets Type As are predisposed to heart disease, cancer, and diabetes. It is particularly important for sensitive Type As to get their foods in as natural a state as possible: fresh, pure, and organic. When you get on the Type A Diet, you will naturally be thinner. If you are accustomed to eating meat, you’ll lose weight rather rapidly in the beginning as you eliminate the toxic foods from your diet. And when you follow the Type diet, you can supercharge your immune system and potentially short-circuit the development of life-threatening diseases.
-When Type As eat meat, they experience sluggishness. Type As have low stomach-acid content, therefore they have a hard time digesting meat. Since Type As eat very little animal protein, nuts and seeds supply an important protein component.
-Type As also thrive on the vegetable proteins found in beans and legumes, except those mentioned for the “Avoid” list. These beans can cause a decrease in insulin production, which may cause obesity and diabetes. Tofu should be a staple in the Type A Diet.
-Dairy foods are also poorly digested by Type As, and can cause metabolic slowdown. Type As can tolerate small amounts of fermented dairy products such as yogurt, kefir, nonfat sour cream, and cultured dairy products.
-Vegetables are vital to the Type A Diet, providing minerals, enzymes and antioxidants. Type A are very sensitive to the lectins in potatoes, sweet potatoes, yams, cabbage, tomatoes and peppers. They aggravate the delicate stomach of Type A. Type A should eat more fruits that are alkaline, avoid mangoes, papaya and oranges for they are not good for your digestive tract.

Blood Type Diet – Type B

-The sturdy and alert Type Bs are usually able to resist many of the most severe diseases common to modern life, such as heart disease and cancer. In fact, a Type B who carefully follows the recommended diet can often bypass severe disease and live a long and healthy life. Types Bs are more prone to immune-system disorders such as multiple sclerosis, lupus, and chronic fatigue syndrome.
-The Type B Diet is balance and wholesome, including a wide variety of foods.
-For Type Bs, the biggest factors in weight gain are corn, buckwheat, lentils, peanuts and sesame seeds. These foods have different lectin that affect the efficiency of the metabolic process, resulting in fatigue, fluid retention, and hypoglycemia. The gluten lectin in wheat germ and whole wheat products also adds to the problems cause by other metabolism-slowing foods.
-It is important to leave off chicken for Type Bs. Chicken contains a Blood Type B agglutinating lectin in its muscle tissue, which attack the bloodstream and potentially lead to strokes and immune disorders.
-Type Bs thrive on deep-ocean fish, but should avoid all shellfish. The shellfish contain lectins that are disruptive to the Type B system.
-Type B is the only blood type that can fully enjoy a variety of dairy foods. Most nuts and seeds(especially peanuts, sesame seeds and sunflower seeds) are not advised for Type Bs., they contain lectins that interfere with Type B insulin production.
-Wheat is not tolerated well by most Type Bs. They contain a lectin that reduce insulin efficiency and failure to stimulate fat “burning”. Rye contains a lectin that settles in the vascular system, causing blood disorders and potentially strokes. Corn and buckwheat are major factors in Type B weight gain, they contribute to a sluggish metabolism, insulin irregularity, fluid retention, and fatigue.
-Eliminate tomatoes completely from Type B diet. It has lectins that irritate the stomach lining. Fruits and vegetables are generally well tolerated and should be taken generously.

Blood Type Diet – Type AB

-Multiple antigens make Type ABs sometimes A-like with weak stomach acid, and sometimes B-like with genetically programmed for the consumption of meats. Type AB do best when their muscle tissues are slightly alkaline. Type ABs can’t metabolize meat efficiently because of low stomach acid, so it is important to watch the portion size and frequency. Chicken has lectin that irritates the blood and digestive tracts of Type ABs also. Tofu is a good protein supplements for Type ABs. Nuts, seeds, beans and legumes present a mixed picture for Type ABs. Eat nuts and seeds in small amounts and with caution.
-Type ABs can tolerate dairy foods fairly well. But watch out for excessive mucus production.
-Generally Type ABs do well on grains, even wheat, but keep in mind that the inner kernel of the wheat grain is highly acid forming in the muscle for Type ABs. Type AB benefits from a diet rich in rice rather than pasta.
-Type ABs has a weaker immune system, so you will benefit from the vegetables, which are high in phytochemicals and the more alkaline fruits, which can help to balance the grains that are acid forming in the muscle tissues. Tomatoes do not impose any ill effects on Type ABs.
-Type AB should begin each day by drinking a glass of warm water with the freshly squeezed juice of half a lemon to cleanse the system of mucus accumulated while sleeping.
What are you waiting for my friends, devise your own blood group diet now for healthy lifestyle and longer life span. :))

MASHAMBULIO YA ANGA YASAMBARATISHA KIKUNDI CHA KIISLAM CHA ISIS

 
Mkuu wa jeshi nchini Marekani Jenerali Martin Dempsey amesema kuwa mashambulizi ya angani dhidi ya kundi la Islamic State yameliharibu kundi hilo,lakini akaonya kuwa kampeni hiyo ya angani pekee haiwezi kuliangamiza kundi hilo.
Amewaambia waandishi habari kwamba kampeni ya nchi kavu dhidi ya kundi hilo ni muhimu nchini Iraq na Syria.
Jenerali Dempsey amesema kuwa kati ya wapiganaji elfu kumi na mbili na elfu kumi na tano kutoka kwa makundi ya upinzani nchini Syria watahitajika katika vita vya nchi kavu nchini Syria.
Idadi hiyo ni mara mbili na hata tatu kwa ukubwa ukilinganisha na idadi inayotarajiwa kupewa mafunzo ya kijeshi mbali na silaha na wanajeshi wa Marekani.

SOMA TAMKO LA UKAWA HAPA JUU YA MAAMUZI YA MAHAKA KUU...

 


                                  UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI(UKAWA)
TAMKO LA UKAWA JUU YA AMRI YA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA KUHUSU MAMLAKA YA BUNGE MAALUM

&

RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA ILIYOWASILISHWA
KWENYE BUNGE MAALUM NA MWENYEKITI WA KAMATI YA UANDISHI YA BUNGE MAALUM

Dar es Salaam, 26 Septemba 2014:

Hapo jana tarehe 25 Septemba, 2014, Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa amri kuhusu maombi yaliyofunguliwa na Bwana Saed Kubenea, mwandishi habari mwandamizi na mhariri wa gazeti la Mwanahalisi kutaka Mahakama Kuu itoe ufafanuzi wa mamlaka ya Bunge Maalum kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za nchi yetu. Katika amri yake hiyo, Mahakama Kuu imesema yafuatayo kuhusu mamlaka ya Bunge Maalum:

(a) “Kwamba kuna mgongano katika maana ya maneno yaliyotumika kwenye kifungu cha 25 cha Sheria hiyo kwenye toleo la Kiingereza la Sheria hiyo. Hata hivyo, licha ya mgongano huo, tafsiri sahihi ya maneno ya kifungu hicho ni kwamba:

(i) “Mamlaka ya ‘kujadili na kupitisha masharti ya Katiba inayopendekezwa’ maana yake ni mamlaka ya kutunga na kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa ajili ya kupelekwa kwa wananchi wa Tanzania ili kupigiwa kura ya maoni;

(ii) “Mamlaka hayo yatatekelezwa kwa kutumia Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalum na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Katika kufanya hivyo, Bunge Maalum linaweza kuboresha na/au kurekebisha Rasimu ya Katiba. Mamlaka hayo yanamewekewa mipaka, kama ilivyokuwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, na tunu na maadili ya taifa yaliyopo kwenye kifungu cha 9(2) cha Sheria;

(b) “Mahakama haina mamlaka ya kuamua aina na upeo wa maboresho na/au marekebisho ambayo Bunge Maalum linaweza kuyafanya kwenye Rasimu ya Katiba kwa sababu hilo ni suala la kisiasa na wala siyo la kisheria, ilimradi maboresho na/au marekebisho hayo hayaendi kinyume na matakwa ya kifungu cha 9(2) cha Sheria.”

Uamuzi huu ni muhimu kwa mchakato wa Katiba Mpya kwa sababu zifuatazo:

(1) Tangu kuanza kwa Bunge Maalum mwezi Februari mwaka huu, kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya wajumbe wa UKAWA na wajumbe wa CCM na mawakala wao katika Bunge Maalum kuhusu mamlaka ya Bunge Maalum kama yalivyoainishwa kwenye kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Wakati UKAWA imeshikilia msimamo kwamba mamlaka ya Bunge Maalum yana mipaka kisheria na Bunge hilo halina mamlaka ya kubadilisha misingi mikuu ya Rasimu iliyotokana na maoni ya wananchi, CCM na mawakala wake imeshikilia msimamo kwamba mamlaka ya Bunge Maalum hayana mipaka na Bunge Maalum lina uwezo wa kufanya marekebisho au mabadiliko yoyote kwenye Rasimu ya Katiba. Uamuzi wa Mahakama Kuu unathibitisha usahihi wa hoja ya UKAWA kwamba mamlaka ya Bunge Bunge Maalum yana mipaka kisheria;

(2) Kwa kusema kwamba Bunge Maalum lina mamlaka ya kufanya maboresho na/au marekebisho kwenye Rasimu ya Katiba, Mahakama Kuu imekataa dhana ya CCM na mawakala wake kwamba Bunge Maalum lina mamlaka ya kubadilisha Rasimu ya Katiba. Amri ya Mahakama Kuu haijataja kabisa neno ‘kubadilisha’ ambalo liliingizwa kwa nguvu kwenye Kanuni za Bunge Maalum. Kwa maana hiyo, kanuni ya 3 ya Kanuni za Bunge Maalum inayotafsiri neno ‘hoja’ kuwa ni pamoja na mamlaka ya Bunge Maalum kubadilisha Rasimu ya Rasimu inakwenda kinyume na matakwa ya kifungu cha 25 cha Sheria na kwa hiyo tafsiri hiyo ni batili;

(3) Kama ilivyokuwa kwa Mahakama ya Rufani ya Tanzania katika kesi ya Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Mwanasheria Mkuu iliyokuwa inahusu suala la mgombea binafsi, Mahakama Kuu ya Tanzania imekwepa kutekeleza wajibu wake wa kutenda haki kwa kufuata Katiba na Sheria za nchi kwa kujificha nyuma ya kichaka cha ‘maamuzi ya kisiasa.’ Mamlaka ya Bunge Maalum yamewekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Mipaka yake imewekwa na Sheria hiyo pia. Mahakama Kuu, kama ilivyo kwa Mahakama nyingine zote, ilikuwa na wajibu wa kutafsiri Sheria hiyo kwa kutamka bayana aina na upeo wa mamlaka ya kisheria ya Bunge Maalum kufanya maboresho na/au marekebisho ya Rasimu ya Katiba. Badala ya kutekeleza wajibu wake huo, Mahakama Kuu imekwepa lawama za CCM na mawakala wake kwa kusema kwamba aina na upeo wa maboresho na/au marekebisho ya Rasimu ya Katiba utategemea matakwa ya kisiasa, yaani ya CCM na mawakala wake, badala ya kutegemea lugha ya Sheria yenyewe. Aidha, Mahakama Kuu imekwepa lawama za UKAWA kwa kukubali hoja kwamba mamlaka ya Bunge Maalum yana mipaka, hata hivyo bila kuifafanua mipaka hiyo;

KATIBA MPYA INATENGENEZWA KWA MTUTU WA BUNDUKI!!!


Hali ya kisiasa katika nchi yetu kwa sasa ni tete kwa kiasi kikubwa. Nchi yetu sasa iko chini ya utawala wa kijeshi usiokuwa rasmi. Kila mahali katika makao makuu ya mikoa, wilaya na majimbo, askari wa Jeshi la Polisi wakiwa na mabomu na risasi za moto, magari ya deraya, farasi na mbwa wametanda kila mahali ili kujaribu kuzuia maandamano na mikutano ya wananchi wanaopinga mchakato wa Katiba unaoendelea.

Mjini Dodoma, Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo linatumiwa na Bunge Maalum limezingirwa na vikosi hivyo vya Jeshi la Polisi. Katika hali hii, ni wazi kwamba mchakato wa Katiba umekuwa mateka wa Jeshi la Polisi, Bunge Maalum lenyewe ni mateka na Watanzania wote ni mateka wa Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya mabavu. Katiba mpya inatengenezwa kwa mtutu wa bunduki. Katika hali tete kama hii, kitu cha ajabu kabisa ni kwamba Rais Jakaya Kikwete – kama ambavyo imekuwa kawaida yake sasa – amekimbia nchi na kwenda Marekani kwa ziara ya wiki mbili.

Kama ambavyo UKAWA imesema katika kipindi chote hiki, chochote kitakachotokana na mchakato huu wa kimabavu hakitakuwa na uhalali wowote wa kisiasa. Sasa, baada ya mabadiliko mbali mbali ya Kanuni za Bunge Maalum kuruhusu uchakachuaji sio tu wa Rasimu ya Katiba bali pia uchakachuaji wa maamuzi ya wajumbe waliobakia wa Bunge Maalum, ni wazi pia kwamba chochote kitakachotolewa na Bunge Maalum kwa sura ya Katiba inayopendekezwa kitakuwa batili kisheria vile vile.

Kwa sababu hizo, tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema na nchi yao kupinga nchi yetu kugeuzwa kuwa dola ya kipolisi na nchi ili chini ya utawala wa kijeshi usio rasmi. Tunawaomba wanachama na viongozi wote wa vyama vya UKAWA kufanya maandalizi ya kupinga vitendo hivi kwa njia mbali mbali za kidemokrasia. Aidha, wanachama na viongozi wetu wafanye maandalizi kwa pamoja kwa ajili ya Uchaguzi wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliotangazwa kufanyika tarehe 14 Desemba, 2014. Uchaguzi huo uwe ni fursa ya kwanza ya kuiondoa CCM katika utawala wa nchi yetu kabla ya kuiondoa kabisa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.



Mh. Freeman Aikaeli Mbowe

MWENYEKITI MWENZA


Mh. Profesa Ibrahim Haruna Lipumba

MWENYEKITI MWENZA



Mh. James Francis Mbatia

MWENYEKITI MWENZA

RIDIWANI AFUNGUKA KUHUSU RAIS KIKWETE SOM HAPA....

JKLabda inawezekana hii ikawa mara yetu ya kwanza kusikia upande wa pili wa President wetu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ambae tumezoea tu kumuona akihutubia, akijumuika na watu mbalimbali kwenye matukio ya furaha na huzuni lakini kuna mengine hatuyajui kuhusu yeye.
Mtoto wake Ridhiwani Kikwete ambae ni mbunge wa Chalinze ameongea kwenye Exclusive na millardayo.com na kueleza ni jinsi gani inavyokua pale ambapo baba yake anakasirika au anapokasirishwa akiwa nyumbani.
Ridhiwani>>>Jambo akiwa halitaki mara nyingi hupenda kusema achana na hilo lakini kama ni mtu kafanya jambo flani sio zuri utamsikia mzee tu anasema huyu mtu bwana achana nae….. maarifa yake madogo, naweza kutoa ushuhuda mbele za watu mzee wangu mimi sio mtu ambae ameishi kwenye mazingira yanayotoa fursa ya matumizi ya lugha ngumungumu kama matusi
‘Yani mtu akimuudhi… huwezi kusikia amefikia hatua ya kutamka labda huyu mshenziiii…. sina kumbukumbu ya mimi kumsikia akitamka neno kama hilo, mara nyingi ukikosea anasema huyu maarifa yake madogo kwelikweli‘ – Ridhiwani

DIAMOND AELEZA KUKASIRISHWA NA SKENDO ZA NDOA NA MENINAH...

      WEMA                                        DIAMOND NA WEMA
                                                                      MENINAH
“Unajua hizi habari kiukweli zimekuwa 
zikinihuzunisha sana,” amesema msanii huyo. “Unajua mie ni mtu mmoja ambaye sipendi kuzunguzia mambo ya rumors, siju magazeti huwa sipendi kuzungumzia kabisa, kwa kuwa najua kabisa siwezi kubishana na media kwakuwa media ni kubwa, maana najua utaongea na huyu na yule siku ya siku utagombana na watu. Ndio maana huwa nakaa kimya,” ameongeza Diamond.

“Kusema ukweli hili suala limekuwa likiniumiza ‘eti sijui kuna vikao vya harusi mie nataka kumuoa Meninah’ Kusema ukweli sina mahusiano na Meninah. Kila mtu anajua mie nina mahisiano Wema. Wema ndo mpenzi wangu, ila wakati mwingine nakuwa naelewa ile inakuwa ni trick ya kibiashara. Mtu anajua hata nikimuandika vipi ‘Diamond sijui kafanya nini watu hawawezi kumchukia! Kwahiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kwa watu kuwa nipo na mwanamke wangu halafu namsaliti.”

“Unajua kitendo hicho hatamaye kinaniudhi naona mtu yupo na mpenzi wake halafu anamsaliti. Najua hicho ni kitendo ambacho kila mtu hakimpendezi. Kwahiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kupitia njia hiyo. Labda wana wasanii wao, sasa wanaona tukiingia kwa njia hii tutaweza kuamharibia Diamond. Ndioa siku zote nimekuwa kimya tu ila sina mahusiano na Meninah. Mie nikiwa na mtu huwa sifichi naweka wazi kabisa. Hata kama leo nimeachana na Wema nasema tu, why nifiche? Mie katika mambo yangu huwa simuogopi mtu kama ningekuwa nataka kuoa basi ninge weka wazi why nifich

Ijumaa, 26 Septemba 2014

ISSA HAYATOU AULA ACHAGULIWA KUWA NAIBU MKUU WA RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA DUNIANI

Rais wa soka duniani Blatter amempitisha aliye kuwa mkuu wa sokabarani Africa(CAF)kuwa naibu mkuu wa shirikisho la soka duniani Mr.issa Hayatou ambaye ni raia wa Cameroon. Hatu ya Blatter kufanya uteuzi huoumekuja baada ya Argentine Julio Grondona aliyekuwa akishikilia wadhifa huo kufaliki dunia mwezi july. Hayatou atakuwa ni mtu wq pili kuwa na maamuzi ya juu katika maswala yahusuyo soka duniani akimfata Blatter.

Jumamosi, 20 Septemba 2014

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amesema kuwa Iran ina jukumu la kutekeleza katika juhudi za kimataifa dhidi ya wapiganaji wa Islamic State nchini Iraq na Syria.
Bwana Kerry ameliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba muungano wa kuliangamiza kundi hilo una majukumu mengine mbali na hatua za kijeshi na kwamba huenda Iran ikashirikishwa.
Wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani imebaini kwamba wawakilishi wa Iran na wale wa Marekani wamejadiliana kuhusu tishio linalosababishwa na wapiganaji hao kandokando ya vikao vya mkutano kuhusu mpango wa nuklia wa Iran.

SIERRA LEONE HAKUNA KUTOKA NJE AMRI ,KUEPUKA EBOLA

Serikali ya Sierra imetoa amri ya kutotoka nje kwa siku tatu.
Lengo la amri hii ni kuhakikisha kuwa kila mtu amekaa nyumbani huku wahudumu wa afya wakiendelea kuwatafuta wagonjwa kwa lengo la kuwaweka karantini ili kuzuia kuenea zaidi kwa Ebola.
Hata hivyo, wakosoaji wamesema amri hiyo itaharibu uhusiano kati ya madaktari na wananchi.
Nchi ya Sierra Leone ni moja kati ya nchi za Afrika Magharibi zilizoathirika sana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huku zaidi ya watu 2,600 wakipoteza maisha yao.
Alhamisi, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa (UN) lilitangaza kuwa mlipuko huo ni tishio kwa usalama na amani duniani.
Baraza hilo liliomba mataifa yote kusadia katika harakati za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.
 
                         Serikali inapania kutumia muda huo kuwatibu wagonjwa
Mvua kubwa iliyoshuhudiwa mjini Freetown hapo Alhamisi haikuwazuia maelfu ya wananchi wa Sierra Leone kwenda sokoni na pia katika maduka ya jumla kununua vyakula vya kutosha kabla ya amri ya kutotoka nje iliyotangazwa na rais kuanza kutekelezwa.
Serikali ya Sierra Leone inaanimi hatua hii itasaidia pakubwa katika harakati za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola ambao umeathiri wilaya 13 kati ya wilaya 14 zilizo nchini humo na kusababisha watu zaidi ya 500 kupoteza maisha yao.
Shirika la madaktari wasio na mipaka wa Medecin Sans Frontieres wamekuwa wakipinga hatua ya kutoa amri ya kutotoka nje, wakisema hatua hiyo itachangia kusambaa kwa ugonjwa huo.
 
                                         Maduka mengi yamebakia yamefungwa
Mwezi uliopita, taarifa kutoka Shirika hilo ambalo wafanyakazi wake wamekuwa wakisaidia katika harakati za kukabiliana na mkurupuko huo, ilisema karatini na amri ya kutotoka nje itasababisha hali ya kutoaminiana kati ya wahudumu wa afya na wananchi nchini humo na kuwafanya wengi kuficha hali zao za kiafya.
Hata hivyo mamlaka nchini humo imesisitiza kwamba hatua hiyo yao itasaidia kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo na kuongeza kwamba watawatuma baadhi ya viongozi kuhakikisha watu hawatoki katika nyumba zao.

Ijumaa, 19 Septemba 2014

HIZI NDIZO NDEGE TANO HATARI DUNIANI ZINAZO MILIKIWA NA URUSI

Japokuwa Urusi inaaminika kuwa na silaha nyingi hatari za kivita lakini mtandao wetu kwa msaada wa mtandao wa yahoo.com unakuletea ndege ambazo ni hatari zaidi zinaposhambulia toka angani zinazomilikiwa na Urusi.
1.PAK FA 

PAK FA.

PAK FA ina rada maalum ya kivita inayosaidia kutazama muelekeo na kuchunguza umbali mrefu kabla ya kufika eneo husika, licha ya uwezo wa kubeba silaha nyingine pia ina uwezo wa kubeba makombora makubwa sita ikiwa ni pamoja na kutupa toka hewani pamoja na ardhini.

PAK kwa mara iliruka hewani kwa dakika 47 January 29, 2010 na baada ya hapo ilifanyiwa majaribio zaidi ya 450 mwishoni mwa mwaka 2013.

Russia inatarajia kutengeneza ndege kama hizo 400 mpaka 450 kufikia mwaka 2020 au 20140 katika mradi ambao inashirikiana na India iliyochangia kiasi cha dola bilioni 6 ili kufanikisha mpango huo.


2.Su-25 FROGFOOT 
Su-25 FROGFOOT. Picha|digitalcombatsimulator.

Ndege hii ina kasi sana na ina sehemu kumi ambazo zinawekwa mabomu ili kushambulia, pia ina uwezo wa kushambulia hewani kwa hewani ikiwa na maana kutungua ndege nyingine hewani na pia kushambulia toka hewani kwenda ardhini. 

Ndege hii ilitengenezwa maalum kushambulia ikiwa karibu na uwanja wa vita si kutoka mbali pia inabeba makombora.

Ndege hii imeshawahi kushambulia Afghanistan mwaka 1979-1989, vita ya Chechnya na sasa hivi inatumika katika mgogoro wa Ukraine.


3.Tu-95 BEAR STRATEGIC BOMBER


Ndege hii ilitengenezwa maalum kwa kurusha mabomu ya nyuklia lakini imekuwa ni vigumu kwa mabomu hayo kutumika kutokana na mpango wa Marekani wa kupinga matumizi ya mabomu hayo hatari Duniani.


Kutokana na kasi yake, ndege hii ilitumika kwenye vita ya baridi kufanya doria kaskazini mwa bahari ya Atlantic pamoja na kuongoza vikosi vya majeshi ya maji. 

Ndege hii kwa sasa ipo katika matengenezo ya kuiboresha zaidi kwa sababu ilitengenezwa miaka 60 iliyopita.


4.Tu-160 BLACKJACK STRATEGIC BOMBER

Ndege hii ilikuwa ni toleo la mwisho mwaka 1980-1992 la Soviet Union kabla haijasambaratika na Russia kumiliki zana nyingi za kivita.


Ndege hii ina uwezo mkubwa wa kufanya shughuli za kivita usiku katika hali zote za hewa huku ikiwa imebeba mzigo mkubwa wa mabomu ya nyuklia pamoja na makombora yenye uzito mkubwa.


Ndege hii ina kasi ya kilomita 2,000 kwa saa pamoja na kutembea umbali wa kilomita 14,000 bila kujazwa mafuta kwa mara nyingine.

Ndege hii pia kutokana na muundo wake ina uwezo wa kugundua kombora lililoelekezwa kwake na kukwepa kabla halijaleta madhara.


5.Su-35 FLANKER FIGHTER
Su-35 FLAKER FIGHTER. Picha presstv.ir.
Ndege hii ina kifaa maalum kinachoweza kumtafuta adui umbali wa kilomita 400 na kumshambulia.

Ndege hii ambayo ina injini mbili pia ina uwezo wa kubeba mzigo mkubwa wa silaha mbalimbali pamoja na maeneo 14 yanayofungwa silaha kwa ajili ya kushambulia.

*Mpangilio wa namba haumaanishi kuwa iliyo namba moja ndio inaongoza au namba tano ndio ya mwisho.



Polisi wapiga waandishi wa habari DarMUENDELEZO wa Jeshi la Polisi nchini kuwanyanyasa, kuwatisha waandishi wa habari na kuwafanya wasitekeleze wajibu wao ipasavyo, ilijidhihirisha wazi jana makao makuu ya jeshi hilo, baada ya waandishi kupigwa, kukimbizwa na mbwa ili wasichukue taarifa za kuhojiwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Tukio la kupigwa na kudhalilishwa kwa waandishi wa habari lilitokea jana, limetokea ikiwa ni siku moja baada ya Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini kushirikiana na waandishi wa habari katika kufanya kazi kwa ajili ya kulinda amani ya nchi.
Waandishi waliyopigwa na Polisi hiyo jana ni Josephat Isango anayeandikia gazeti hili, huku Yusuph Badi ambaye ni mpiga picha wa magazeti ya serikali, akipigwa na ‘kusakiziwa’ mbwa ili wamuume.
Dalili za waandishi wa habari kuzuiwa kufanya kazi yao, zilianza kujionesha mapema jana wakati Mbowe alipowasili katika makao makuu ya Jeshi la Polisi, ambako waandishi walizuiwa wasiingie katika eneo hilo kwa ajili ya kuchukua picha na maelezo ya kiongozi huyo.
Akiwa anawaongoza askari wake katika amri ya kushambuliwa kwa waandishi wa habari hiyo jana, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja, alisikika mara kwa mara akiwaagiza vijana wake wawaondoe waandishi na hata kuwasakizia mbwa.
Chagonja, alisikika mara kadhaa akitoa amri kwa askari kuwa wawafungulie mbwa ili waweze kujeruhi angalau mtu mmoja kutoa funzo ili wafuasi wa CHADEMA waliokuwa kwenye lango kumsubiri Mbowe waondoke.
“Waondoeni wote msiwaruhusu hata hao waandishi kuingia humu, ninyi askari wa mbwa mnafanya nini hapo wakati watu wamejazana mlangoni wapelekeeni hao,” alisikika akisema Kamishna Chagonja.
Mara baada ya maelekezo hayo ya Kamishna Chagonja, askari waliokuwa na mbwa walianza kuwakimbiza wafuasi wa CHADEMA na waandishi wa habari.
Katika hali ya kustaajabisha, askari watatu kwa pamoja walimfuata Josephat Isango, aliyekuwa akitoka katika lango kuu na kuanza kumshambulia kwa rungu na mateke hali iliyowafanya waandishi wa habari kuingilia kati kwa ajili ya kumnusuru.
Baada ya waandishi kumnusuru Isango, kipigo kiligeukia kwa Mwandishi Yusuph Badi, ambaye wakati akishambuliwa alianguka chini huku askari wenye mbwa wakiwaachia kwa ajili ya kumshambulia.
Kilichomnusuru Badi asiumwe na mbwa hao ni kamera aliyoishika mkononi na kujikinga ili asidhurike, kitendo hicho cha kujikinga kilisababisha kuharibika kwa kifaa hicho.
Wakizungumza baada ya hali kutulia, Badi na Isango, walieleza kuwa kilichofanywa na jeshi la Polisi ni kuminya uhuru wa utendaji kazi wa waandishi katika kuuhabarisha umma wa watanzania juu ya mambo yaliyokuwa yakitokea.
“Ni jana tu wameambiwa namna ya kutoa ushirikiano na vyombo vya habari, lakini leo wanatupiga na kutusakizia mbwa hii si haki na viongozi wetu wanapaswa waangalie mara mbili mbili namna ya kushirikiana na jeshi hili,” alisema Badi.
Jeshi la Polisi limekuwa na kawaida ya kuwanyanyasa, kuwapiga na hata kuwaua waandishi wa habari pale wanapotekeleza wajibu wao wa kukusanya habari.
Tukio linalokumbukwa zaidi la ukatili wa askari wa jeshi hilo kwa waandishi wa habari ni mauaji ya Mwandishi wa kituo cha Televisheni ya Chanel ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi, mauaji yaliyotokea Septemba 2 mwaka juzi katika Kijiji cha Nyololo Mufindi mkoani Iringa wakati mwandishi huyo akiwajibika kukusanya habari.


Alhamisi, 18 Septemba 2014

POLISI WA WADHARILISHA WAANDISHI WA HABARI,WAWAPIGA ,WATUMIA MBWA KWENYE MAHOJIANO YA MBOWE NA POLISI JANA.


Siku moja baada ya makamu wa rais dkt mohamed ghalib bila kuhimiza mahusiano mema wakati wa utendaji kazi baina ya vyombo vya ulinzi na usalama na vyombo vya habari jeshi la polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa limekiuka kauli hiyo kwa kuwapiga na kuwajeruhi baadhi ya waandishi wa habari na kuwazuia kutekeleza wajibu wao wakati mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema alipowasili katika makao makuu ya jeshi hilo kwa mahojiano.
Kauli hiyo ya makamu wa rais imeshindwa kutekelezwa kutokana na tukio lililotokea majira ya saa 5 na dk 15 asubuhi wàkati mwenyekiti wa chadema taifa Mhe. Freeman Mbowe alipowasili makao makuu na askari wa polisi  kutaka kuzuia gari alilopanda kuingia ndani ya lango kuu pamoja na waandishi wa habari na watu wengine kuamriwa kuondoka katika eneo hilo agizo lililopingwa na waandishi wa habari na baadhi ya wanasheria wa Chadema.
Kufuatia na kutolewa kwa ilani hiyo jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia-FFU- kilianza kupiga waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wananchi huku wengine wakikimbia kuhofu vipigo toka kwa askari hao ambapo baaadhi ya waandishi walioumizwa sehemu mbalimbali ya mihili yao.
Akiwatangazia wafuasi waliokuwa wakikataa kuondoka katika maeneo hayo mwanasheria wa chadema mhe. Tundu lissu licha ya kuwahakikishia kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa Mhe. Freeman Mbowe yuko salama amewataka kuondoka katika eneo hilo na kurudi majumbani ili kuepusha vurugu na misongamano ambayo ingeweza kusababisha matatizo zaidi.
Aidha ITV imeshuhudia mwenyekiti wa Chadema taifa Mhe Freeman Mbowe akitoka makao makuu ya jeshi la polisi akisindikizwa na ulizni mkali wa jeshi la polisi kuelekea katika ofisi za makao makuu ya chama hicho baada ya kukamilika kwa taratibu za kipolisi.

Jumanne, 16 Septemba 2014

WEMA ATUPIA YOUTUBE VIDEO WAKIFANYA YAO NA DIAMOND.

Wema afanya hivyo ili kuwafunga midomo wahasidi wa penzi lao wanaosema wametengana ,hivyo awaonyesha mambo yanaendelea kama kawaida na Mr.mdogo mdogo.

KIONGOZI WA BROTHERHOOD AHUKUMIWA MAISHA JELA.


 MOHAMED BADIE
Mahakama nchini Misri imemhukumu kiongozi wa kidini wa kundi la Muslim Brotherhood,Mohamed Badie kifungo cha maisha jela,yeye pamoja na wafuasi wake wapatao kumi na wanne.
Badie amehukumiwa kufuatia kukutwa na hatia ya makosa ya mauaji na ukatili na pia kutaka kumng'oa madarakani rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi mnamo mwaka 2013,Badie tayari ameanza kutumikia kifungo hicho .
Hata hivyo mwanaharakati mashuhuri Alaa Abdel-Fattah yeye ameachiliwa huru katika mahakama ingine,Alaa alihukumiwa miaka 15 jela kwa kushiriki katika maandamano ambayo yalizuiliwa mnamo mwaka wa jana.

UKISTAHAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAHUN...SHOGA AJIFUNGUA MTOTO WAKIUME...!!

HII IMETOKEA HUKO NCHINI NIGERIA AMBAPO SHOGA HUYO AMEJIFUNGUA MTOTO WA KIUME.

BOTI YAZAMA YAUWA BWANA HARUSI,WENGINE 17 PIA WAPOTEZA MAISHA.


Takriban watu 17 akiwemo bwana harusi na watoto wawili wamekufa maji baada ya boti ya uokoaji iliyokuwa imewabeba wageni kwenda kwa sherehe ya harusi kuzama katika mafuriko nchini Pakistan.
Maafisa wanasema kuwa takriban watu 22 wameokolewa huku waokoaji wakiwatafuta watu zaidi.
Msemaji wa shirika la kukabiliana na majanga amesema kuwa zaidi ya watu millioni 2 nchini humo waliathiriwa na mafuriko hayo ambayo yalisababishwa na mvua kubwa.
Maafisa wanasema kuwa takriban watu 289 wamefariki katika mafuriko hayo nchini Pakistan kufikia sasa.
Zahid Ali mwenye umri wa miaka 27,mchumba wake Mashal pamoja na wageni walikuwa katika boti hiyo iliyokuwa ikielekea katika sherehe za kundeleza harusi yao.

 
               Watu 18 waliokuwa wanakwenda kushuhudia harusi wameaga dunia
Maafisa wanasema kuwa boti hiyo iliojaa kupitia kiasi ilikuwa ikivuka mto Chenab uliofurika katikati ya mji wa Punjab eneo lililoathirika vibaya na mafuriko nchini Pakistan.
Msemaji wa huduma ya uokozi katika eneo hilo la Punjab amesema kuwa familia hiyo ilionywa kuhusu mafuriko hayo.
Bi harusi amesema kuwa alinusurika baada ya kushika mti wa stima.
Mazishi ya waathiriwa 17 yamefanyika huku waokoaji wakiendelea kuwatufuta wale waliotoweka.

HUYU NDIYO HAMISA MABETO ATUPIA PICHA YA NUSU UCHI INSTA.....MCHEKI HAPA!


SLAA AENDELEA KUULA,MNYIKA KUMRITHI KAMBWE,MWALIM ZANZIBAR.....!

Chama cha CHADEMA kimeendelea na uchaguzi wake mkuu wa kuteuwa viongozi wa ngazi za juu ambapo Freeman alishinda kuwa Mwenyekiti,Prof,Safari makamo wa Bara na Side wa Zanzibar.
Kutokanana na katiba ya chama hicho kumtaka Mwenyekiti kuteuwa Katibu Mkuu,Naibu Katibu Mkuu wa Bara na wa Zanzibar ,Mbowe amemteuwa Dr.Willbrod  Slaa kuwa Katibu Mkuu wa chamahicho huku nafasi ya Zitto Kabwe akipewa  Mnyika na kwa Zanzibar ameteuliwa Salum Mwalim.
                   ANGALIA PICHA ZA WALIOTEULIWA HAPA.


                             SLAA KULIA,MNYIKA KATIKATI NA MWALIM KUSHOTO

HIZI NDIZO STORY ZILIZO KWENYE MAGAZETI YA LEO JUMANNE 16 SEPT,2014